Burudani
RECAP: Diamond ametoa somo la kufanya Promo – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia namna msanii Skylatylaa alivyoandaa Tour katika majiji 17 kwa ajili ya Promo ya Wimbo wa Bombshell.
Anasema katika Somo wasanii wetu wanatakiwa kuiga ni namna ya kufanya Promo katika Kazi zao hasa nyimbo na album.
Tour katika majiji 17 duniani na bado anasema ataongeza mengine ni kuonyesha jinsi gani wasanii wetu hawafanyi kazi Promo za ngoma zao.
Inawezekana wanataka kufanya lakini bajeti hawana, jambo hilo linachangia sana muziki wetu kusua sua.
Kama Diamond atakuwepo kwenye hiyo Tour maana yake ataendelea kuutengeneza ukubwa wake kimuziki Kimataifa.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.