Burudani

RECAP: Diamond apata Show 2 Paris na London “Headliner”

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia kuhusu Jina la Diamond kukosekana kwenye Tamasha la Afro Nation litakalofanyika Urene mwezi wa 7.

Anasema sio Diamond tu bali Wizkid, Asake, Rema na wengine wakubwa hawapo kwenye Orodha ya wasanii watakaotumbuiza Ureno.

Anasema katika Post ya Afro Nation mashabiki wengi wamehoji wasanii hao kutokuwep Ureno lakini wanasahau kuwa Tamasha hilo hufanyika mara mbili kwa mwaka.

Afro Nation hufanyika Ureno na Marekani hivyo mara nyingi wanaokosekana Ureno basi hutumbuiza Marekani, hivyo Diamond na wengine wanaweza kutumbuiza Marekani.

Mbali hiyo Diamond amepata Show mbili Paris Ufaransa katika Tamasha la AFRO DOM FEST litakalofanyika siku mbili.

Siku ya kwanza yeye ndio atakuwa muongoza Show na siku ya Pili ni DadJu, baada ya hapo ana show London tena tarehe 13 yaani wiki moja baadae.

Kwa sasa kuna Namna Diamond amejipata Kimataifa, hata kama akikosa Tamasha moja basi atapata Tamasha lingine kubwa.

Kwa muziki wa Bonho Fleva tunatakani kuona wasanii wengi wakitumbuiza Kimataifa isiwe Diamond pekee.

Uchambuzi mzima Upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

Cameraman @samirkakaa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents