Burudani

RECAP: Diamond apongezwe kufungua WCB – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia namna lebo za

muziki zinavyokufa taratibu kisa biashara mbovu.

Anasema Lebo ya WCB ndio ilifunguliwa kwa lengo la kusaidia wasanii na kufanya biashara ya muziki na ndio maana unaona lebo zingine zinakufa yenye imesimama.

Diamond ndio alikuwa anajua sababu ya kufungua lebo na alishajifunza namna ya kusimamia lebo ila wengine wakafuata

mkumbo bila kuijui biashara kiundani na wakataka

kushindana naye.

Matokeo yake lebo zao haziingizi chochote, wanawanyanyasa

wasanii wao, Uwekezaji hakuna na wasanii wao hawapati shows ambazo zitawatengenezea pesa.

Kwenye upande huu lazima tumpe maua yake Diamond na kama kuna msanii anataka kufungua lebo aende kwake

akajifunze namna lebo zinavyosimamiwa.

Ukiangalia kwa sasa Konde Gang Chali, Next Level Chali, Kings Music haieleweki wasanii wao hakuna wanachofanya kimuziki, uwekezaji hakuna maana yake ile lebo haipo hai kwa sasa.

Biashara ya lebo inahitaji uwekezaji mkubwa sana hasa ukiwa na wasanii wengi, tusifanye kama sifa kujionyesha kuwa

tumekuwa wakubwa, ukweli ni kwamba wasanii wengi

walifuata mkumbo.

Uchambuzi mima upo katika akaunti yetu ya Youtube

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents