Burudani

RECAP: Diamond msanii pekee anayekuza thamani ya muziki wetu – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amefafanua kwa urefu zaidi namna Diamond anavyokuza thamani ya muziki wa Bongo Fleva.

Anasema kuwa vyote anavyofanya Diamond sio kwa faida yake tu bali kwa faida ya kiwanda kizima cha muziki.

Wasanii wenye wanaeleza namna Diamond alivyoanza kukataa show akitaka kulipwa milioni 10 lakini baadae wote walikubali.

Kwa sasa amebadili lifestyle, kwenda kwenye Show ni Private Jet na kulipwa mabilioni ya pesa, itafika muda kuna wasanii watafika level hizo.

Ukitoka nje ya Tanzania, watu wahisi wasanii wetu wana maisha mazuri kama Diamond vyote ni kwa sababu ya Thamani yake, maana yake hata thamani ya muziki wetu inapanda.

Kuna mataifa yanahisi wasnaii wote Bongo wanatumia Private Jet kama Diamond kumbe laaa, lakini picha anayoijenga nje inatupa Thamani.

Uchambuzi mzima Upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

Cameraman @samirkakaa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents