RECAP: Diamond&Zuchu wakiachana hawawezi kutangaza Biashara yao (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameizungumzia kauli ya ZUCHU kuwa ameachana na DIAMOND.
Anasema kuwa ni ngumu sana DIAMOND kuachana na ZUCHU kwa sababu ya kulinda biashara yake ambayo ni ZUCHU.
Anaongeza kuwa siku Diamond akiachana na Zuchu watu hawatajua ila ukiona wanatangaza ujue kuna project inakuja na watu wanatakiwa kuizungumzia.
Yale aliyoandika Zuchu inawezekana yapo kwenye wimbo kwa sababu Diamond hawezi kuruhusu kuharibu biashara yake kamwe.
Anasema kuwa Ikitokea kweli Diamond ameachana na Zuchu atauathiri muziki wa Zuchu kwa asilimia kubwa sana kwa sababu namna Diamond alivyomtengeneza Zuchu kwa watu ni kupitia mahusiano yao.
Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive
Cameraman and Editor @samirkakaa