RECAP: Eddy Kenzo, Savara & Zuchu wamefanya Show mbovu CHAN – El Mando
Kupitia kwenye kipindi chake cha @recap_mando @el_mando_tz amezungumzia Show za Wasanii walizofanya kwenye fainali za CHAN Nairobi Kenya.
Anasema watu wengi wanamzungumzia Zuchu tu akiongelewa yeye pekee yake kwamba kafanya Show mbovu bali ni wasanii wote waliotumbuiza siku ile.
Anasema bado inaonyesha wasanii wengi hawawezi kihimili Show za Uwanjani hasa kwenye majukwaa ambayo yanehusisha mechi za mpira.
Anaongeza kuwa watu wengi pia wanajaribu kulalamikia miundombinu kwa mataifa yetu kwamba mibaya kwa wasanii kufanya Show za Viwanjani.
@el_mando_tz anasema yeye anapingana nao kwa sababu kuna wasanii wamewahi kufanya Show za Uwanjani kwenye mechi za mpira na wakifanya show kubwa sana katika viwanja vile vile.
Amemtolea mfano Alikiba katika Show yake ya SimbaDay aliimba LIVE kabisa na sauti ilisikika vizuri lakini pia Show ya Alikiba ya Super League kati ya Simba na Al ahly.
Msanii mwingine ni Diamond Platnumz wakati Uwanja wa Amani Unazinduliwa, alifanya Show kubwa sana na sauti ilisikika vizuri tu.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman @johnbosco_mbanga






