RECAP: EP ya Mbosso imetoba mbele ya Show za Diamond, Dabi ya Simba & Yanga – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameendelea kuizungumzia EP ya Mbosso kwa kusema imefanikiwa kupenya katika matukio makubwa sana.
Ep yake imefanikiwa kwenye kila eneo, Numbers, Challenges, Engagemnet, kupendwa na mashabiki na Promo yake imekuwa kubwa.
Kuanzia ngoma ya kwanza mpaka ngoma ya 7 zote zimekuwa ngoma pendwa na kila mtu ana ngoma yake anayoipenda.
Wakati Mbosso anaachia EP kulikuwa na mambo mengi sana yanaendelea ikiwemo Shows za Diamond London, Manchester, Glasgow na Summer Jam na kila kitu kilichofanyika nje.
Baadae ya muda Diamond na Harmonize wakaachia ngoma zao kwa wakati mmoja mitandao ikachafuka.
Vyote hivyo havikuzuia Ubora, Ukali wa EP ya Mbosso, mambo mengi yaliendelea lakini EP ya Mbosso ikabaki kukamata mitandao yote.
Sio hayo tu kwenye mpira sakata la SIMBA na YANGA kucheza au kutocheza likawa kubwa sana mitandaoni lakini halikuweza kuizima EP ya Mbosso.
Kwa bahati ngoma ya AVIOLA ikapita na Upepo wa YANGA kuwa Bingwa, kwenye upande wa Promo Yanga wakamsaidi Mbosso kwa kiasi kikubwa.
Yote hayo yamepita lakini EP ya Mbosso bado ya moto, inawezekana wasanii wengi wanawaza namna ya kutoa Ngoma ziwe kubwa kama EP ya Mbosso.
Amefunika Ngoma zote zilizotoka baada ya EP yake, Yeye ndio kalikamata GAME kwa sasa. Kila kona ni PAWA au AVIOLA.
Alipo Diamond anajipiga KIFUA..! YESS NIMEKUZA JEMBE LINGINE, Ni Alarm kwake, asivimbe kichwa na kuridhika.
Uchambuzi mzima Upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman & Editor @samirkakaa & @mbanga