Burudani

RECAP: Hakuna Matata yazua Taharuki Uingereza (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumza namna Komasava ya Diamond na Hakuna Matata ya Marioo zinaisumbua Afrika.

Amesema kuwa kwa sasa muziki wa Amapiano ndio muziki Bora duniani sio tu Afrika, hata wasanii Davido na Burna boy wamefanya Remix ya Tswala Bam.

Kwa upande wa Afrika Tanzania inauwezekano mkubwa ikawa ndio taifa la pili kwa kuzalisha muziki mzuri wa AMAPIANO baada ya Afrika Kusini.

Muziki huu upo juu ya AFRO BEAT ya Nigeria kwa sasa, hivyo msanii akifanya Amapiano basi hufuatiliwa zaidi.

Anaongeza kuwa ukitaja nyimbo tano bora Afrika kwa sasa huwezi kuzitoa Komasava & Hakuna Matata, ukipita kwenye page ya mchezaji wa timu ya wanawake ya MANCHESTER UNITED amelitumia neno HAKUNA MATATA.

Mchezaji huyo anaitwa @millieturner neno ambalo ni la Kiswahili, kuna muda utafika BONGO FLEVA itakuwa namba moja duniani.

Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

Host: @el_mando_tz
Cameraman: @samirkakaa

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga b

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents