
Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameizungumzia Collabo mpya ya Harmonize aliyowashirikisha Rapa wa Marekani Bobby Shmurda pamoja na Bien kutoka nchini Kenya.
@el_mando_tz anasema kabla ya kuangalia ngoma itakuwa heat au itabuma kwanza tuangalie juhudi alizofanya kumpa Bobby Shmurda pamoja na Bien.
Anaongeza kuwa Harmonize apongezwe sana kwani ameanza kutimiza malengo ya kufanya kazi na wasanii wakubwa duniani.
Inawezekana huu ukawa mwanzo tu na Collabo hii kama Atai-promote vyakutosha inaweza kumfungulia milango Kimataifa zaidi.
Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi kwenye hili??