Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari

RECAP: Harmonize mwaka 2024 hana wimbo wa kufanyia Tour Kimataifa – El Mando

RECAP: Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameizungumzia kauli ya Harmonize kutangaza kuwa anakuja na album ya Kombe la Dunia.

Anasema kuwa Harmonize amekubali kuwa album yake iliyopita ni hasara na ndio maana ametangaza ujio wa Album nyingine.

@el_mando_tz anasema kuwa kauli hiyo ya Harmonize inaonyesha kuwa amekubaliana na haki na kuamua kuanza upya mwaka huu kwa kuja na album nyingine.

Harmonize ni msanii anayejikubali na asiyeogopa kuanguka na kuanza upya, Album hiyo amesema kuwa atashirikisha wasanii tofauti kutoka kila kona ya dunia.

Album hiyo ikitoka huenda ikatikisa duniani kote lakini @el_mando_tz ameongeza kuwa Harmonize kwa mwaka huu mpaka sasa hana wimbo utakaomfanya awe na jeuri ya kufanya Tour Kimataifa.

Hilo ni deni kwake, ajitahidi atoe ngoma ambayo itamfanya afanye Tour Kimataifa kitu ambacho ni lazima kwa msanii kama Harmonize.

Mpaka sasa Harmonize wa mwaka 2024 huwezi kumfananisha na Harmonize wa mwaka 2023 na 2022, mwaka huu kashuka kiasi fulani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents