Burudani

RECAP: Hela ya Alikiba ipo kwa Vanillah

Kupitia kwenye kipindi chake pendwa cha RECAP & MANDO leo @el_mando_tz amemzungumzia msanii kutoka lebo ya Kings Music chini ya Alikiba Vanillah.

@el_mando_tz amesema kuwa licha ya Vanillah kuachia wimbo mpya wa Sijazoea lakini ameshathihirisha mara nyingi sana kuwa uwezo wake ni mkubwa sana.

Ukiachia mbali ngoma ya UTU ambayo ni uandishi wake lakini pia kwenye collabo kadhaa na wasanii wenzake ameonyesha umahiri wake.

@el_mando_tz anasema kuwa licha ya watu wengi mitandaoni kuamini kuwa ni kama Alikiba anamtengeneza Baraka The Prince mpya ila Vanillah ana kipaji cha hali ya juu sana.

Unahisi Alikiba anamtengeneza Baraka Mpya?? Na Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents