RECAP: Huu ndiyo utofauti wa Alikiba na Diamond Spotify (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz leo amezungumzia wasanii 10 wanaopata wasikilizaji wengi zaidi kwenye mtandao wa Spotify.
Anasema kuwa wasanii wa Kenya wanaonekana wadogo kimuziki Afrika Mashariki lakini wana numbers kubwa sana kwenye mtandao wa Spotify.
Anaongeza kuwa msanii namba moja anaitwa @sofiyanzau ambaye anapata Monthly Listerners milioni 10 na msanii wa pili ni Diamond ambaye anapata Monthly Listerners milioni 1.7.
Tofauti ya msanii wa kwanza mpaka wa pili ni kubwa sana na hiyo ni ishara tosha kuwa muziki wetu au wasanii wetu wanapata numbers chache sana kule.
Katika Top 4 wasanii wa Kenya wapo watatu huku Tanzania ikiwakilishwa na msanii mmoja pekee amabye ni Diamond.
Umahisi kwanini Wasanii wa Tanzania wapo chini zaidi Spotify kuliko wasanii wa Kenya??
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman & Editor @samirkakaa