Bongo5 ExclusivesBongo5 MakalaBurudaniDiamond PlatnumzMuziki

RECAP: Ibraah na Vanillah wanazidi kujishusha (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameizungumzia ngoma mpya ya Vanillah wa Kings Music na Ibraah wa Konde Gang.

Amewapongeza kuwa kutengeneza numbers Audimack ndani ya masaa nani tu na kufanya Collabo ambayo wengi waliamini ni ngumu.

Ukija kwenye upande wa wimbo wao, kwa level zao na ukubwa wao Hakunaga ni wimbo wa kawaida mno, kwa namna mashabiki walivyokuwa na hamu ya kuona wanafanya kazi pamoja kwa namna moja ama nyingine hawajaitemdea haki collabo yao.

Anaongeza kuwa Ibraah na Vanillah kwa namna watu wanavyowachukulia mtaani wangetoa ngoma moja kubwa sana ila ukweli ni kwamba hawajaitendea haki collabo yao.

Leo hii hata Alikiba na Harmonize hawawezi kujivunia collabo ya wasanii wao eti kwamba collabo kubwa.

Anasema kitu kimoja wasanii wa kizazi hiki wamekosa ni kufanya muziki wenye ushindani wao kwa wao bali wanafanya muziki wa kawaida mno.

Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

 

 

 

Cameraman and editor @samirkakaa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents