Burudani

RECAP: Kenya watashinda Grammy kabla ya Bongo – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz anasema Muziki wa Kenya umeanza kuamka tena baada ya kusua sua kwa miaka kadhaa.

Ukiangalia mwenye upande wa Wasanii wa kuimba ubora wao umeongezeka sana ukiwatolea mfano watu kama Sauti Sol akiwemo Bien lakini pia Bensoul na wengine.

Ukija mwenye upande wa Hip Hop Khaligraph Jones anazidi kupambana kwa nafasi yake na Hip Hop ya Kenya ipo kwenye mikono salama.

Kwa Tanzania ukiwatoa Diamond na Alikiba ambao wao kwa sasa hawafanyi tena muziki wa Ushindani zaidi maana wameshafanikiwa hawana kitu cha Ku-Prove hatuna wasanii wengine level zao.

Hii inatoa ishara mbaya sana kwa game ya Bongo Fleva maana wasanii wa Kenya wamejua wapi Watamzania wanakosea au Udhaifu wao upo wapi.

Anaongeza kuwa Taifa la Kenya litakuwa taifa la Kwanza kwa msanii wao kushinda GRAMMY tofauti na Tanzania maana wasanii wa Tanzania hawajawekeza kwenye Quality ya muziki.

Ametolea mfano BIEN ana Tour yake Marekani na Ulaya.

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents