RECAP: Komasava itamsumbua Diamond kupata wimbo wa kuifunika (Video)
Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezizungumzia Show za Diamond Ujerumani na Barcelona lakini pia Show ya Mabantu Ujerumani.
Anasema kuwa shangwe ambalo wasanii wetu wamepata inatupa picha kuwa muziki wetu unakua na kuna sehemu nzuri umefika mpaka sasa.
Mbali na hilo amesema kuwa Komsava itampa shida sana Diamond lupata Hit nyingine itakayoifunika na kwa level aliyofikia anatakiwa ameze kubaki kwenye level ya kutengeneza Hit kama Komasava ili aendelee kukuza jina Kimataifa.
Anaongeza wasanii wengi wakitoa hit huwa wanapata tabu kupata Hit nyingine kwenye mwendelezo huo huo na mara nyingine ngoma zinazofuata baada ya hit huwa za kawaida.
Anaongeza kuwa ili aweze kujaza kumbi kubwa kama 02 ARENA LONDON lazima atoe ngoma zinazofuatana kubwa kama Komasava.