BurudaniDiamond Platnumz
RECAP: Lavalava & D Voice ni Biashara zilizofeli WCB?? – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amejibu na kufafanua wale wanaosema D Voice na Lavalava ni biashara zilizofeli pale WCB.
Haya yamekuja baada ya Diamond kutangaza kusaini msanii mpya katika lebo yake ya WCB na baadhi ya mashabiki kuanza kusema kuwa:-
Diamond ameamua kusaini msanii haraka baada ya Biashara ya D Voice kufeli katika lebo yake ya WCB, wengine wameenda mbali na kusema pia Lavalava.
Kwa upande wake @el_mando_tz amefafanua na kusema kkuna asilimia kadhaa wapo sahihi na zingine hawapo sahihi.
Amefafanu kwanini mashabiki wanahisi vile.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman & Editor @samirkakaa