Burudani

RECAP: Lavalava hana mafanikio kimuziki atoke nje ya WCB – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia sakata la Lava lava kudaiwa kumaliza mkataba katika lebo yake ya WCB.

Asema Baba levo huwa anazungumza kama masihara lakini mwishowe yanakuwa kweli, hata kwa Mbosso ilikuwa hivi hivi.

@el_mando_tz anasema kama kweli Lava lava kamaliza mkataba, kwa upande wake anamshauri aondoke WCB akajitegemee.

Anasema kuna namna Lava lava kivuli cha WCB kinambeba sana kimuziki lakini pia kimfunika na aonekana ni msanii aliyefeli ndani ya WCB.

Anasema Level iliyosetiwa WCB inaonekana kabisa Lava lava ameshindwa kuimuda maana wasanii kadhaa wamemkuta WCB lakini Kimafanikio ya Kimuziki wamemzidi.

Mfano mdogo tu Mbosso na Zuchu, wao ndio walimkuta WCB lakini kwa sasa huwezi kuwafananisha wamempita mbali sana.

Anasema sio kwamba Lava lava hana kipaji au hatoi ngoma kali, mwishowe kwenye maisha kuna kitu kinaitwa Bahati, huenda Lava lava hana bahati na WCB Hivyo akitoka anaweza kufanikiwa zaidi.

Lava lava anaweza kupata show nyingi sana ambazo ni level yake lakini kuwa WCB kuna Standard iliyowekwa na ni ngumu level hiyo Lava lava kuifikia na ndio maana hatumuoni kwenye Shows kwa sasa.

Akiondoka ana uwezo wa kufanya Shows nyingi na kupata madili mengi kutokana na level yake.

Uchambuzi mzima Upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

Cameraman @samirkakaa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents