BurudaniDiamond Platnumz

RECAP: Lebo nyingine zimekufa lakini WCB bado – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia taarifa za Diamond kutangaza kusaini msanii mpya katika lebo yake ya WCB.

Anasema kwa namna Diamond anavyoiendesha lebo yake inafaa apewe heshima kubwa sana maana sio rahisi kuendesha lebo na ikasimama.

Tuna ushahidi wa lebo nyingi Tanzania kwa sasa zimebaki majina tu na zina baadhi ya wasanii lakini hakuna Progress yoyote inayoendelea zaidi ya wasanii kujiamulia wanavyotaka.

Sio tu hiyo WCB ndio lebel pekee inayokuza msanii na kumfikisha lwenye mafanikio makubwa zaidi kuliko lebo yoyote Afrika Mashariki na ushaidi huo tunao kwa Harmonize, Rayvanny, Mbosso.

Kutangaza kuwa amesaini msanii mpya maana yake anakuja Harmonize au Rayvanny mwingine, hiyo habari ni njema sana kwa sababu tutaona kipaji kipya.

Kwa sasa Kiwanda Cha Bongo Fleva hakukuzi wasanii wapya, wamebaki wale wale tu na lebo zingine kwa sasa hazina dalili ya kusaini wasanii wapya WCB pekee angalau.

Anaongeza kuwa kwa Afrika nzima WCB ni lebo namba mbili au namba tatu baada ya Mavins Record ya DonJazz na YBNL NATION ya Olamide.

Uchambuzi mzima Upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

 

Cameraman & Editor @samirkakaa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents