Bongo5 ExclusivesBurudaniDiamond PlatnumzFahamuHabari

Recap & Mando: Diamond kum-kiss Fantana, Zari kukasirika uhalisia au Script??

Kupitia kipindi cha RECAP na MANDO @el_mando_tz amefannya uchambuzi wa Show ya Alikiba aliyoifanya pamoja na Ayra Starr siku ya Jumamosi hii katika ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar Es Salaam.

@el_mando_tz amezungumzia vitu kadhaa ikiwemo mpangilio wa ndani ya ukumbi ulivyokuwa lakini kubwa zaidi kuhusu show yenyewe ambayo ilikuwa ya wasanii wawili tu.

Alikiba ni miongoni mwa wasanii ambao ni alama kubwa sana kwenye muziki wa Bongo Fleva linapokuja suala la kuimba live.

@el_mando_tz ameonngeza kuwa kitu alichokifannya Alikiba wikiendi hii ni alama tosha kuonyesha kuwa kuimba live inabaki kuwa kitu muhimu kitakachomfanya msanii apenndwe jukwaani.

“Siku zote mashabiki wanapolipia kiingilio kwenye show yako huwa wanatarajia kitu special kwa sababu kama ni muziki huwa wannausikiliza kwenye radio na hata video wanaziona mitandaoni, unapoandaa show lazima uwe nna kitu cha kitofauti cha kufanya jukwaani”

Alichokifanya Alikiba nndio kitu ambacho kinamtofautisha yeye na wasanii wengine ambao likija suala la kuimba live huwa ni kitendawili kwao.

@el_mando_tz amemaliza na sababu zinazowafanya wasanii wasiimbe live jukwaani.

Mbali na hayo kupitia kipidi cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ametusanua kuwa kile kilichofanywa na Diamond na mwanadada Fantana kwenye Young Famous & Africans ni Script (imetengenezwa)

Ametoa sababu zake kuwa hakuna kitu kitaonekana kwenye movie bila kupangwa na huenda hata Zari alikuwa anajua nini kinaendelea kwenye movie.

Kitendo cha Zari kuja mtanndaoni na kuandika huenda ni maelekezo au wameshauriana na Diamond kwa lengo la kutanngaza biashara yao (Reality show) yao.

@el_mando_tz ameongeza kuwa siku zote Diamond anabaki kuwa mfalme wa Kiki Afrika Mashariki, msanii pekee mwenye uwezo wa kutengeneza Attention na kila mtu akaannza kumfuatilia.

Baada ya tukio lake hilo na Zari kila mtu alianza kuwazungumzia wao na kuacha kuongelea kingine, hata show ya Alikiba na Ayra Starr kuna namna fulani watu hawakuipa sikio.

Kibiashara kwa diamond inaenndelea kumuweka kwenye njia salama sana kwa sababu anauza bidhaa zake vizuri kabisa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents