RECAP: Mbosso msanii wa kwanza kutoka WCB na kutrend bila Kiki – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amempongeza Mbosso na Uongozi wake kwa kuja na mpango kazi ambao umefanikiwa kwa asilimia kubwa.
Ni mara chache sana msanii atoke WCB halafu akafanikiwa kwa ukubwa ule aliofanikiwa Mbosso baada ya kutoka WCB na EP yake kupokelewa kwa ukubwa.
KITU GANI HUCHANGIA WENGI WASIFANIKIWE WAKITOKA WCB???
Majibu ni kwamba WCB hufanya Uwekezaji mkubwa sana kufikia hatua kwamba ukiwa mwenyewe huwezi kuwekeza kufikia level waliyokuwa wanawekeza WCB.
Hapo ndio wasanii wengi hushikwa na pressure na kuonekana muziki umewashinda kitu ambacho ni tofauti na Mbosso.
Mpango kazi wao ulikuwa kuja na EP na ku-prove mbele ya Jamii kuwa Mbosso anauwezo wa kujisimamia mwenyewe na kuweza kufika mbali.
Mpango kazi wa pili ulikuwa ni kufanya muziki wenye ubora ambao utapokelewa kwa asilimia kubwa na mashabiki wa muziki nchini.
Mpango kazi wa tatu kufanikiwa kwenye upande wa Promo, kila mtu awe free kufanya promo ya EP na pia wa-enjoy muziki mzuri.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman & Editor @samirkakaa & @johnbosco_mbanga