Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari

RECAP: News ya Darassa na Marioo ina mapungufu haya – El Mando

RECAP: Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameizungumzia ngoma mpya ya Darassa na Marioo ya News.

Anasema kuwa sio kawaida ya Darassa na Marioo wimbo wao kutoka na kuwe kimya mitandaoni kwa kiasi hiki, inaonyesha mashabiki hawajaupokea vizuri wimbo wao wa News.

@el_mando_tz anasema inawezekana Upepo wa Komasava umesababisha wimbo huu usizungumziwe sana Mitandaoni na kutofanya vizuri au bado mapema??

Anaongeza kuwa licha ya wimbo huo ambao ulisubiriwa kwa hamu kutokufanya vizuri au kutopokelewa vizuri lakini pia kwa upande wa Viewers wapo chini sana.

Inawezekana Timing ya wimbo inekuwa sio sahihi?? Inawezekana hawajafanya Promo au huenda wamezoeleka sana??

Unahisi kwanini wimbo huu hauna mapokezi mazuri mtaani??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents