Burudani

RECAP: Nuhu Mziwanda kumtafuta Mama Dangote kisa Diamond sio sawa, BASATA wamsaidie – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia sakata la msanii Nuh Mziwanda kuomba msaada kwa wasanii wenzake.

Anasema ukitazama namna Nuh Mziwanda anavyolalamika mitandaoni utagundua kuwa hayupo sawa, ana Stress huenda kuna mengi yanamsibu.

Anahitaji msaada sio wa Wimbo bali msaani wa kimawazo na msaada wa kifedha, hata akipewa Collabo bado atahitaji msaada mwingine.

Anasema Nuh Mziwanda asiwalaumu wasanii wenzake maana kila mtu anapambana na maisha yake.

Watu pekee wa kumsaidia Nuh Mziwanda ni BASATA maana ndio walezi wa wasanii nchini.

Haitakiwi ifike muda msanii apoteze maisha ndio wajitokeze, kazi ya BASATA ni kuwasaidia wasanii kwa namna yoyote ile na sio kuwaita wanapotoa nyimbo zisizo na maadili tu.

Lazima wawe mstari wa mbele kama walezi wa wasanii kujua Nuh Mziwanda anahitaji nini?? Yupo sawa Kiafya?? Watafute namna ya kumsaidia msanii wao na sio kuwatupia lawama wasanii wenzake.

Uchambuzi mzima upo Katika akaunti ya YouTube ya Bongofive.

 

 

 

 

Cameraman@samirkakaa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents