RECAP: Pengo la Aidan kwa Alikiba ni kubwa – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amemzungumzia Staa wa Bongo Fleva Alikiba kwa kuhoji kwanini hajatoa ngoma mpaka sasa.
Anasema kuwa Alikiba alitanga kuachia ngoma yake mpya ya
UBUYU ila mpaka sasa siku 15 zimepita bado kimya na hajatoa Taarifa yoyote.
Anaongeza kuwa Alikiba kwa sasa anafanya kazi bila meneja na huenda ikawa sababu ya baadhi ya vitu vya Alikiba kutokuwa wazi kwa mashabiki zake.
@el_mando_tz anasema Alikiba anahitajika kutoa wimbo hakuna namna, tangu atoa EP yake ya Starter ni miezi 9 imepita kitu ambacho sio kawaida yake.
Kukaa bila ngoma imepelekea Kushuka kwa Numbers zake kwenyw Digital Platforms kitu ambacho kinasababishwa na msanii huyo kukosa ngoma inayofanya vizuri.
Anaeleza kuwa kukosekana kwa ngoma kali ya Alikiba inapeleka kukosekana kwenye Shows nyingi na namba kushuka, hivyo ili arudi juu inamlazimu kutoa ngoma.
Fanbase yake bado kubwa lakini mashabiki wanahitaji nyimbo ili aendeleee kuilinda fanbase yake.
Uchambuzi mzima Upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman@samirkakaa