RECAP: Rayvanny mkubwa kuliko Harmonize & Alikiba Kimataifa – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha @recap_mando @el_mando_tz ameizungumzia Interview ya Rayvanny na kusema mengi sana ameongea ambayo watu walikuwa hawayafahamu.
Rayvanny amezungumzia kuanzia alipotoka WCB Kiasi cha pesa Alicholipa kuondoka WCB na mengine mengi sana kuhusu maisha yake.
Kubwa zaidi ametaka atoelewe kwenye orodha ya BIG4 na kusema hataki kuwepo kwenyw hiyo orodha maana anaona anasharauliwa tu.
Rayvanny pia alijibu kuhusu wanaosema kashuka kimuziki, alisema kama Nimeshuka Kimuziki msanii gani kapanda na amenipita sehemu gani??
@el_mando_tz anasema ukweli ni kwamba Rayvanny ni msanii namba mbili kwa Ukubwa Afrika Mashariki baada ya Diamond Platnumz.
Rayvanny ndio msanii ambaye anamkaribia Diamond kwa mafanikio yake ya Kimataifa na hata upande wa Numbers.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman @johnbosco_mbanga






