Bongo5 ExclusivesBurudaniDiamond Platnumz

RECAP: Rayvanny ndio Msanii mwenye mafanikio zaidi Bongo?? (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amemzungumzia msanii wa Bongo Fleva Rayvanny kuwa huenda ndio msanii mwenye mafanikio makubwa zaidi Tanzania.

Ametaja baadhi ya fact zinazoonyesha Rayvanny ndio anafanikio makubwa zaidi kuliko msanii yoyote Tanzania kwa kuanzia na Streams zake Spotify kupitia TETEMA ndio anaongoza akiwa na milioni 42.

Pia amesema Rayvanny ndio msanii pekee kushinda tuzo ya BET kutoka Tanzania na kingine ndio msanii pekee yeye na S2kizzy kuwa Nominated kwenye tuzo kubwa za GRAMMY.

Ameenda mbali zaidi akisema Rayvanny huenda akaungana na Diamond kwa kupanda majukwaa makubwa zaidi duniani lakini pia kwa upande wa Youtube Kusini mwa Jangwa la Sahara yeye ni msanii wa pili kwa kuwa na Subscribers wengi YouTube.

Rayvanny amewapita Burna boy, Wizkid, Davido, Harmonize na Alikiba, yeye akiwa na zaidi ya Subscriber milioni 5 huku Diamond akiwa na milioni 9.

Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive

 

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents