Burudani

RECAP: Roma na Madee wamsaidie Jose Mtambo

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia kauli za Roma na Madee kutaka Q Chillah na Jose Mtambo wasipewe Interview na Media.

Anasema kauli hizo za Madee na Roma zimekaa kibaguzi sana maana wakihojiwa ndio jamii inajua aina ya changamoto wakongwe wanazopitia.

Ukweli ni kwamba Jose Mtambo ana hali mbaya ya Kiafya kwa namna mahojiano yalivyokuwa anahitaji msaada kutoka kwa Jamii.

Roma na Madee wanaposema wanyimwe Mahojiano na Media tafasiri yake ni kwamba wanataka jamii isijua maisha wanayoishi wasanii wao na je watasaidika vipi??

Biashara ya muziki ilivyokaa inawanufaisha wachache sana kwenye game ilia asilimia kubwa wanaishi maisha magumu sana, jamii inatakiwa kujua.

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents