RECAP: Sallam Sk hana Mkataba na Diamond?? (Video)
Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameizungumzia ngoma mpya ya AY, FID Q na YOUNG LUNYA ya Drop It.
Anasema wakongwe kama wataamua kuwa serious hivi kwenye muziki kama walivyofanya kwenye ngoma yao basi tunaweza kuiona Hip Hop ya Tanzania ikarudi kwenye Ramani ya muziki tena.
Anaongeza kuwa kutokana na kauli ya Sallam Sk kuwa hana Mkataba wa kazi na Diamond Platnumz basi kuna haja asimamie wasanii wengine ili wawe wakubwa pia.
Sallam Sk ni mdau anayelijua game la Bongo Fleva vizuri kwa maana hiyo anaweza kuchukua msanii yoyote akamsimamia na akawa mkubwa kimuziki.
Kuna haja ya kufanya hivyo ili amtengeneza Diamond mwingine hata asimamie msanii wa Hip Hop mmoja tu ili game lichangamke tena la Hip Hop.
Kama Sallam Sk hana mkataba wa kazi na Diamond unahisi kwanini hajasimamia msanii mwingine??
Uchambuzi mzima Upo kwenye akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman & Editor @samirkakaa