RECAP: Ukweli kuhusu ugomvi wa Juma Lokole na Zuchu, familia innahusika??

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia ugomvi wa Mtangazaji wa Wasafi Juma Lokole na msanii wa WCB ZUCHU.
Anasema kuwa moja ya kitu kilichomshangaza ni kuona Zuchu anagombana na mtu ambaye sio msanii na haoni hasara yoyote kwenye ugomvi.
Anasema Juma Lokole anaonekana ana sapoti kubwa sana nyuma ya ugomvi ule maana anapata wapi nguvu ya kugombana na mpenzi wa Boss wake.
Anaongeza Zuchu awe makini asitokea kwenye reli maana bado anahitaji kuifanyia Promo album yake, anatakiwa kuwekeza muda mwingine kwenye muziki wake na namna ya kufanya Promo album na sio Ugomvi.
Ugomvi wao unamfaidisha zaidi Juma Lokole kwa sababu anapata Content lakini kwa upande wa Zuchu unampotezea muda kwa sababu ataacha kufanya muziki na kuhangaika na mambo ya mitandaoni yanayompotezea muda.
Anaongea Mpaka sasa Diamond anatakiwa aingilie kati maana panaelekea pabaya maana Zuchu ni biashara yake na Juma ni mfanyakazi wake.