RECAP: Video ya Msumari ya Diamond ni kali, wimbo wa kawaida kwake- El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha @recap_mando @el_mando_tz ameizungumzia ngoma mpya ya Diamond ya
Msumari aliyoiachia Jumatatu.
Anasema Diamond anafundisha nini maana ya uwekezaji kwenye video, Msumari imetendelewa haki na Diamond, Bideo Vixen na Direcotr Folex.
Hil video itaingia katika orodha ya video bora za mwaka 2025, Uandishi wa Diamond umetukuka sana na hiyo inadhihirisha ukali wake kwenye uandishi.
Ingawa nyimbo za namna hii kwa Diamond ni vitu vya kawaida kwake, haimaanisha nyimbo mbaya ila kwenye uandishi wa
Diamona MSUMARI sio kwamba ndio ngoma aliyoandika zaidi.
Kwa ukubwa wake, huu ni wimbo wa kawaida sana maana ana ngoma ambazo aliwahi kuandika sana siku za nyuma, lakini pia nyimbo za aina hii kwa Diamond huwa haziendi mbali sana.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman @johnbosco_mbanga






