RECAP: Wanaomponda Said Said kuchekesha mbele ya Rais ni Chuki – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia sakata la mchekeshaji Said Said kuchekesha mbele ya Rais Samia.
Ametoa maoni yake baada ya watu wengi kumponda na kusema kuwa amekosea alivuka mipaka na wengine kusema ameanza kulewa sifa.
Kwa upande wake ametoa maoni na kusema kuwa Said Said kwenye upande wa Content alizozungumza hajakosea chochote na kitu alichokosea ni ile cheni kumpelekea
Mhe.Rais tu.
Watu wengi wanaomponda Said Said hawajui maana ya
Comedy na ndio maana Rais alikuwa anafurahia Comedy ila wanaomponda ni mitandaoni.
Anaongeza laiti Said Said angevuka mipaka angeshushwa Stejini, lakini kwa sababu wanajua ni vichekesho na ni utani ndio maana hawajamuakbia chochote.
Wanaolalamika hawajazoea vitu hivi, mwanzoni walimsifia ila leo wamemponda, inawezekana wengi wameanza kuchukia mafanikio yake maana sio rahisi Kumchekesha Rais.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube