RECAP: Wasanii wanavyotengeneza Pesa Spotify (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz eo ametoa elimu ya bure namna wasanii na nyimbo zao zinavyoingiza pesa Spotify, Itunes na Apple Music kwa kila Streams.
Anasema kuwa kwa namna nyimbo zinavyoingiza pesa wasanii wachache sana Tanzania wanatengeneza pesa kwa ukubwa na wengine bado hawanufaiki.
Anasema Spotify Streams moja ni dola 0.003-0.004 huku Itunes na Apple Music ni dola 0.01 per streams, Spotify Streams lakini moja unalipwa dola 400 na Streams milioni moja unalipwa dola 4,000.
Lakini pia Streams hizo zinategemeana taifa na taifa, sio kila taifa linalipa Sawa kwa mataifa kama Marekani na Ulaya tofauti na mataifa ya Afrika na mabara mengine kwa malipo kuna (Freebot na Streamers)
Ukienda upande wa Itunes na Apple Music wanalipa Streams milioni moja ni dola 7,000 kwa wimbo, anauliza kwa Tanzania wasanii wanagapi wana uwezo wa kutemgeneza numbers kubwa kule??
NB: Streams zinatofautiana gharama ya Streams kuna malipo ya Freebot na malipo ya kulipia App (Streamers) katika kila Taifa.
Jibu lake ni kwamba wachache mno.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman & Editor @samirkakaa





