RECAP: Watu maarufu waliokufa Bongo waandaliwe Walk of Fame ya heshima (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia kuhusu watu maarufu walioigusa jamii wapewe heshima.
Anasema kuwa kuna haja ya kuandaliwa eneo la kiheshima la watu waliopoteza maisha ambao waliigusa jamii kwa namna moja ama nyingine.
Anatolea mfano watu maarufu waliopoteza maisha na waliigusa jamii kama Ruge Mutahaba, Reginad Mengi, Amina Chifupa, Steven Kanumba na wengi na kusema watu hawa wamepewa heshima wapi??
Je mtu akitaka kumjua Ruge Mutahaba ni nani au Reginad Mengi ni nani Taarifa zake wanazipata wapi?? Na kwa namna walivyoigusa jamii wapi wamepewa heshima??
@el_mando_tz anatoa ushauri kwa Mamlaka kuwa waandae sehemu ya kuwapa heshima watu waliougusa jamii hata vizazi vijavyo wapate Taarufa zao.
Anachoongea @el_mando_tz ni jambo la msingi au lipuuziwe halina msingi?? Na Unakubaliana nae kwa asilimia ngapi??
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Camerman & Editor @samirkakaa