AfyaBongo5 ExclusivesBurudaniFahamuHabariLifestyleMakalaMarimba Music ChartMichezoSiasaTechnologyTragedy
RECAP: WCB ndio lebo inayokiuza wasanii zingine zinapoteza wasanii – El mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz anasema kwa sasa Tanzania lebo zimekuwa nyingi mpaka zimeharibu thamani ya neno lebo.
Lebo zimekuwa nyingi na haijulikani zinafanya kazi gani maana hakuna lebo hata moja inayokuza wasanii imebaki lebo moja tu ya WCB ndio inakuza wasanii.
Anasema imekuwa kama sifa kwa wasanii wetu wakiaminishwa kwamba ili uwe mkubwa kimuziki fungua lebo kumbe uongo.
Hakuna uwekezaji unaofanyika wasanii wanapoteza vipaji vyao badala ya kuwa wakubwa.
Ameitolea mfano WCB inavyokuza wasanii kama Harmonize, Rayvanny, Mbosso, Zuchu, Lavalava lakini ukienda kwenye lebo zingine hali ni mbaya.
Kama hawawezi kuwekeza kwanini wanafungua lebo?? Ni sifa au kitu gani??