Burudani

RECAP: Willy Paul anamuhitaji Diamond zaidi kimuziki – El Mando

bongofive Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia mashabiki wengi kumkataa Willy Paul kwenye collabo na Phina kisa sakata lake na Diamond.

Anasema baada ya Willy Paul kuona hizo comment alikuja na kusema hana shida na Watanzania bali msanii wetu alitaka kumletea dharau na yeye hapendi dharau na kusema anawapenda Watanzania na wanahitajiana.

Ukweli ni kwamba Tanzania na Kenya wanahitajiana sana kwenye biashara ya muziki na mambo mengine ila Willy Paul kwa ujumbe wake bado anaonyesha ana kinyongo na Diamond.

Kwa ukubwa wa Diamond Willy Paul anamuhitaji zaidi Diamond kuliko Diamond kumuhitaji Willy Paul, kwa maana hiyo Willy Paul anatakiwa kuwa Humble sana kwa mtu kama Diamond.

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

 

 

 

Cameraman@samirkakaa

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents