AfyaBongo5 ExclusivesBurudaniFahamuHabariLifestyleMakalaMarimba Music ChartMichezoSiasaTechnologyTragedy
RECAP: Yafahamu mapungufu kwenye video ya Zuchu ya Anthena (Video)
Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameizungumzia ngoma mpya ya Zuchu Anthena aliyoiachia video yake juzi.
Anasema kuwa Zuchu ameonyesha uwezo mkubwa sana kwenye upande wa Ubunifu na amepitia kwenye njia za Michael Jackson kwenye wimbo wa Thriller
Anasema kila kitu kina mapungufu yake hata Anthena ya Zuchu ina mapungufu kadhaa ikiwemo kuweka INTRO ndefu zaidi yenye dakika 1 na sekunde 10.
Anasema hiyo Intro ni ndefu sana kwenye wimbo mmoja ingawa pungufu hilo haliondoi ubora wa wimbo na Ubunifu mkubwa uliotumika mule.