RECAP: Zuchu amezungumziwa kuliko mechi ya Fainali ya CHAN – El Mando
Kupitia kwenye kipindi chake cha @recap_mando @el_mando_tz amezungumzia tukio lililotokea Wakati Zuchu anafanya Show kwenye fainali za CHAN.
Anasema wakati Show inaendelea baadhi ya Wakenya wakawa wanaimba Wimbo wao wa Taifa badala ya kufuatilia Show ya Zuchu.
Wengi wanafai Zuchu aliwakataa Wakenya na wao wanalipiza kitu ambacho kauli hiyo imepingwa na lebo yake ya WCB kwamba ni Taarifa za Uzushi.
Anasema Wasanii wanapaswa kuwa makini sawa na maneno yao, wasiwe wanatoa Comment kwenye mambo yanayoendelea mitandaoni.
Anaongeza Wakenya kumkataa Zuchu sio hasara kwa Zuchu bali kibiashara amefanikiwa kwa asilimia kubwa kwani amezungumziwa zaidi kuliko hata wasanii wenzake waliotumbuiza CHAN.
Anasema kibiashara ina faida kubwa sana kwa Zuchu kuliko hasara maana kila kona amekuwa story na ni kitu chenye faida kwa msanii hata kama akizungumziwa vibaya.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman @johnbosco_mbanga





