RECAP: Zuchu asingetoa Inama, Diamond angekaa kwenye Amanda – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha @recap_mando @el_mando_tz ameizungumzia ngoma mpya ya Zuchu na Diamond ya INAMA.
Anasema katika kitu Zuchu amekosea ni kuachia wimbo huo muda huu wakati anatakiwa kuendelea kuipa nguvu na nafasi ngoma ya AMANDA.
Anasema Zuchu kupitia Wimbo huo ni kama amerudi nyuma hatua kadhaa kwani tayari alitoa wimbo wenye sound na Ubora wa Kimataifa ila amekuja kutoa wimbo local.
Anasema kumuweka Diamond kwenye wimbo wa INAMA amekosea bali angetakiwa kumshirikisha Diamond kwenye wimbo wa AMANDA Remix.
Mara nyingi collabo za Diamond na Zuchu huwa haziendi mbali sana hasa hufanya vizuri kwenye mataifa yanayoongea Kiswahili.
Katika wimbo ambao angetakiwa aupe muda ni AMANDA walau atoa Remix mbili tatu na pia atoe hata video yake hapo alikuwa na nafasi ya kuachia wimbo mwingine.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman @johnbosco_mbanga






