Bongo MovieBongo5 ExclusivesBurudaniDiamond PlatnumzMuziki

RECAP:Willy Paul atakufa Kimuziki (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameeleza kushangazwa na mashabiki wanaomshindanisha Msanii wa Kenya Willy Paul na Diamond Platnumz.

Anasema kuwa mashabiki wanaomshindanisha Willy Paul na Diamond hawamkuzi kimuziki bali wanataka kumuua kimuziki.

Anasema Willy Paul atakuwa anafanya kazi kuangalia Diamond kafanya nini na itafika muda ataharibu mipango yake na kutaka kufanya anachokifanya Diamond, hapo ndio utakuwa mwisho wake.

Anamshauri kuwa Willy Paul abaki kwenye njia na mipango yake asikubali mashabiki wamtie Pressure kutaka kushindana na Diamond.

Anasema ili kuamini hilo kuna muda Mashabiki walimjaza upepo akatoa wimbo umeandikwa Simba ingawa aliufuta.

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

Cameraman and Editor @johnbosco_mbanga

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents