
Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria Divine Ikubor alimaarufu Rema, usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kushinda tuzo katika wimbo wake aliomshirikisha staa wa muziki kutoka Marekani Selena Gomez kupitia ngoma yao ya ‘Calm Down’ Rema na Selena wameshinda tuzo ya “Best Afrobeats” kupitia Remix ya ngoma hiyo katika tuzo za MTV Video Music Awards hizo zilizofannyika New Jersey, Marekani.
Rema ameshinda tuzo katika kipengele kilichokuwa kinawaniawa na wakali kama Ayra Starr kupitia Rush, Burna Boy kupitia It’s Plenty, OBO Davido featuring Musa Keys kupitia Unavailable, Fireboy DML & Asake kupitia Bandana Libianca – “People”, Rema & Selena Gomez – Calm Down, Wizkid featuring Ayra Starr– 2 Sugar.
Wakati anaongea baada ya kushinda amewashukuru wasanii wenzake wa Nigeria ambao amesema kuwa wamekuwa wakumsapoti sana mpaka kufika hapo alipo lakini pia amemshuruku Selena Gomez kwa nafasi ya kufanya anye kazi.