Republican waingiwa na hofu kuhusu Tik Tok

Kundi la Maseneta wa Chama Cha Republican nchini Marekani hapo jana waliweka shinikizo dhidi ya mtandao wa kijamii wa Tik Tok, likiutaka utawala wa Rais Donald Trump kutathmini kitisho kwamba app hiyo inayomilikiwa na China ya kusambaza video huenda itaingilia uchaguzi wa Marekani.

US government agencies are banning TikTok, the social media app ...

Katika barua jana, Marco Rubio. Tom Cotton na wabunge wengine walielezea madai ya uchujaji taarifa unaofanywa na Tik Tok wa maudhui nyeti, ikiwa ni pamoja na video inayokosoa China inavyowatendea Waislamu wa kabila wa Uighur ambao ni wachache pamoja na madai ya jaribio la Beijing kuvuruga majadiliano ya kisiasa katika app hiyo ya mtandao wa kijamii.

Wabunge hao waliandika katika barua hiyo kuwa wana wasi wasi mkubwa kwamba chama tawala cha Kikomunist cha China kinaweza kutumia udhibiti ilionao wa Tik Tok kuvuruga ama kushawishi mazungumzo ili kusababisha mgawanyiko miongoni mwa Wamarekani na kufanikisha lengo lao kisiasa.

Related Articles

Back to top button