Video: Rick Ross alimaliza beef la Drake na Meek Mill

Rick Ross, ambaye ni boss wa Maybch Music Group, amefunguka na kusema kwamba, amekaa chini na Drake na kuzungmza, na hatimaye ku ‘squash’ beef iliyokuwepo baina ya Drake na msanii aliyechini yake Ross, Meek Mill.

Rick ross amesema kwamba, alikua analitazama beef hilo kwa muda mrefu, tangu lilipoanza lakini alishindwa kutia neno, kutokana na Darke kuwepo kwenye label ya Cash Money, na heshima yake kwa label hiyo inayomilikwa na Birdman. Alisema kwamba hakutaka kuingilia kwani label ya Cash Money ilikua inapitia mvutano ambao alitaka kuona mwisho wake ni upi na hatimaye sasa kuamua kukaa chini na Drake mwenyewe kuyamaliza.

“Huu ni muda wa kutafuta pesa, na hata nilivyokaa na dogo, tuliongelea issues positive za jinsi ya kuongeza kipato na pia kuhakikisha kwamba beef yake na Meek Mill inaisha. Ni muda wa kuwaza ‘nine figures’ na namna ya kuzipata, na sio beef.” alisema Ross.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=7jAD75_SGTU[/embedyt]

Insadikika kamba, beef ya Drake na Meek Mill ilitokana na mahusiano ya Meek na Nicki Minaje kumkers Drake, kwani Drake amesikika mara kwa mara akifunguka ya moyoni jinsi anavyompenda nakumtamani Minaj ambao wanatoka kundi moja la Young Money (YMCMB).

Related Articles

Back to top button