Rihanna aivunja rekodi hii ya Michael Jackson

Rihanna ameivunja rekodi iliyowekwa na Michael Jackson kwakuwa msanii wa tatu aliyetoa nyimbo nyingi zilizoshika nafasi ya kwanza.

rihanna

Single mpya ya muimbaji huyo mwenye miaka 28, Work aliyomshirikisha Drake, imekuwa ya 14 kukamata nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot 100 na kumshinda Michael aliyekuwa na nyimbo 13.

Rihanna bado yupo nyuma ya Mariah Carey, mwenye nyimbo 18 huku The Beatles wakishika rekodi ya dunia kwa kuwa na nyimbo 21.

Related Articles

Back to top button