BurudaniHabari

Rihanna aupania usiku wa Super Bowl, nina miaka 7 sijapanda jukwaani

Mashabiki wa Rihanna wanatarajia kwa hamu kubwa ya kushubiria onyesho la msanii wao katikati ya mchezo wa Super Bowl – mojawapo ya tafrija kubwa na ya kifahari katika muziki.

Mwimbaji huyo atatumbuiza wakati wa mapumziko wakati wa mchezo kati ya Philadelphia Eagles watakapochuana na Kansas City Chiefs siku ya Jumapili.

Rihanna ameeleza kuwa ana takribani miaka 7 hajawahi kupanda jukwaani kutoa burudani yoyote.

 

Mashabiki wanatumai kuwa onyesho la Rihanna katika mchezo huo wa Super Bowl la mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 34 linaweza kuashiria kurudi kwake tena kwenye muziki baada ya kuwa kimya kwa muda.

 

“Sijapanda jukwaani kwa miaka saba,” alisema, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mchezo huo mkubwa.pia ameongeza “Unapokuwa mama kuna kitu ambacho hutokea tu ambapo unahisi kama unaweza kuchukua ulimwengu, unaweza kufanya chochote.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents