BurudaniUncategorized

Ripoti: Diamond na Mavoko kukaa meza moja kuzungumza tofauti zao bila mameneja wa WCB

Alhamisi hii tulishuhudia kikao kizito kilichochukua zaidi ya masaa 2 kati ya uongozi wa WCB, Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) pamoja na muimbaji Rich Mavoko ambaye anadaiwa kuingia kwenye mgogoro wa kimaslahi na uongozi wa label hiyo unaongozwa na muimbaji, Diamond Platnumz.

Hatua hiyo imekuja baada wiki mbili zilizopita muimbaji huyo kupeleka mkataba wake katika baraza hilo baada ya kuona kuna mambo hayaendi sawa, na ndipo baraza hilo lilipoamua kumuita Diamond ili kuzungumza naye kuhusiana na sakata hiyo, na baadaye wakaitwa wote kwaajili ya kuwekwa sawa kama ilivyofanyika jana.

Diamond na mameneja wake wakaa zaidi ya saa moja wakimsubiri Rich Mavoko.

Kikao hicho cha jana kilichofanyika katika ofisi ya Basata chini ya Katibu Mtendaji, Godfrey Mngereza kilitakiwa kuanza majira ya saa 6 mchana lakini kilichelewa kidogo kuanza kutokana na Rich Mavoko kuchelewa kufika eneo la tukio huku dada yake pamoja na shangazi yake akiwahi.

Diamond pamoja na mameneja wake wawili, Babu Tale na Sallam wakifika eneo la tukio majira ya saa 5 na robo asubuhi huku Rich Mavoko alichelewa kufika eneo la tukio kwa zaidi ya saa moja ambapo ilifanya dada yake, Dokii kuzungumza na wanahabari kuhusiana kuchelewa kwa muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo, Ndegele ukiwa ni wimbo wake wa kwanza toka aondoke WCB.

“Rich yupo njiani anakuja, amechelewa kidogo kutokana na masuala ya foleni lakini mara kwa mara nazungumza naye kwahiyo kuweni na subira,” alisema Dokii.

Lakini baada ya saa moja, Rich Mavoko aliingia BASATA akiwa na gari jeusi kama unavyoliona kwenye video hapo juu na kwenda moja kwa moja ofisi za baraza hilo na kupokewa na Afisa Matukio ya Sanaa wa baraza hilo, Bwana Malegesi.

Mameneja wa WCB, Tale na Sallam pamoja ndugu wa Mavoko waondolewa kwenye kikao.

Baada ya kikao kuanza na kukaliwa kwa zaidi ya dk 45, walionekana mameneja wa WCB, Babu Tale, Sallam SK pamoja na ndugu wa Rich Mavoko wakitoka ndani ya kikao hicho. Ndani ya kikao hicho alibaki Diamond Platnumz, Rich Mavoko pamoja na watumishi wa Basata akiwemo, Katibu Godfrey Mngereza.

Sallam aliimbia Bongo5 kwamba waliondolewa kwenye kikao hicho kwa kuwa hakiwahusu, kwahiyo wameachwa wahusika ambao ni Diamond pamoja na Rich Mavoko ili wazungumze wao kwa wao kwa sababu ni wasanii.

“Mazungumzo yapo vizuri, kwa sasa ndani wamebaki Rich na Diamond wale ni wasanii, mimi sio msanii, ukikuta kuna baraza la mamejena Diamond atatoka nitabaki mimi,” alisema Sallam.

Aliongeza “Hakuna kitu kigumu duniani, kwahiyo ndio maana nikasema hebu tuwaache wazungumze halafu wakitoma tutaambiwa wamezungumza nini kwa sababu sisi sio wasemaji,”

BASATA, Rich Mavoko pamoja na Diamond wala kiapo cha kutozungumza walichojadiliana.

Baada ya kunalizika kwa kikao Diamond na Rich Mavoko alitoka kwa pamoja kila mmoja aliwa na lake. Waandishi wa habari kama kawaida yao kujaribu kuzungumza na wasanii hao ili kujua kilichojadiliwa ndani lakini wasanii wao walishindwa kuzungumza chochote.

Nao Basata walishindwa kueleza nini walizungumza na wasanii hao na kuacha maswali mengi kwa wadau na wapenzi wa burudani ambao walitaka kujua nini kimejadiliwa na kama tofauti zao zimemalizika.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, kimedai Diamond na Rich Mavoko watakaa kikao chao binafsi bila mameneja wao weekend hii na wiki ijayo watarudi tena Basata kwaajili ya kutoa taarifa ya kile walichozungumza na ndipo baraza hilo litoe taarifa rasmi.

Wadau wa mambo wanadai huwenda wakizungumza wawili bila watu wengine watamaliza tofauti zao na kuendelea kufanya kazi kama awali kwani tatizo lao sio kubwa sana kama baadhi ya watu wanavyofikia.

Related Articles

13 Comments

  1. Me sioni mantiki yoyote hapo mana najua kabla hujasaini mkataba lazima usome mkataba ndo usaini sasa inakuaje hapo mtu anasaini halaf kakaa mwaka naa anasema ananyonywa ina mana alisaini bila kusoma mkataba wasanii wa bongo acheni kukurupuka

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents