HabariSiasa

Rishi Sunak Waziri Mkuu mpya Uingereza

Mwanasiasa wa Uingereza Rishi Sunak amechaguliwa hii leo kuwa kiongozi wa chama chga Conservative na atakuwa waziri mkuu ajaye, baada ya mshindani wake Penny Mordaunt kujitoa katika dakika za mwisho.

Sunak ambaye ni mmoja wa wanasiasa tajiri zaidi nchini Uingereza, na ambaye atakuwa kiongozi wa kwanza wa taifa hilo asiye Mzungu, na muumini wa dini ya Kihindu, ataombwa na Mfalme Charles III kuunda serikali, na kuchukuwa nafasi ya Liz Truss, aliedumu katika nafasi hiyo kwa siku 44 tu kabla ya kujiuzulu.

“Kama afisa wa uchaguzi katika mchakato wa uongozi, naweza kuthibitisha kwamba tumepokea uteuzi halali mmoja tu. Hivyo, Rishi Sunak amechaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha Conservative,” alisema Sir Graham Brady, mwenyekiti wa kamati yenye ushawishi ya 1922.

Katika taarifa ya kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho muda mfupi kabla ya kutangazwa mshindi, Penny Modaunt ameutaja ushindi wa Sunak kama uamuzi wa kihistoria, ambao kwa mara nyingine umeonyesha uanuwai na kipaji ndani ya cha chama chao, na kuongeza kuwa anamuunga mkono Rishi kikamilifu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents