Burudani

RnB haifanyi biashara vizuri, haiuzi – Ben Pol

Msanii wa muziki Bongo, Ben Pol ameeleza sababu ya waaimbaji wengi wa RnB kutofanya vizuri Bongo.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Zai’ amesema muziki wa Rn B unahitaji uvumilivu kwa sababu haufanyi vizuri sokoni na ndio kitu ambacho kinawashinda wengi.

“RnB ni muziki ambao unahitaji mtu uwe na passion kwa sababu asilimia kubwa ya miziki ya RnB haifanyi biashara vizuri, haiuzi . Kwa hiyo wale wachache wanaofanya kwa moyo na kubadilisha kidogo na kuifanya Kitanzania, wanaimba kiswahili fasafa, unaona kina Jux, Rama Dee, Ben Pol wanaweza kufanikiwa kuwafikia watu,” amesema.

“Lakini wengine wanaingia kwa mkumbo kwa kujaribu ndio wanashindwa wanaingia kwenye miziki mingine ambayo ndio inaonekana unauza hapo hapo, hata hao wengine inadoda pia,” Ben Pol ameiambia Dj Show ya Radio One.

Ben Pol ameshinda tuzo kadhaa kupitia muziki wa RnB ambao amekuwa akiufanya kwa kipindi kirefu sasa. Mwaka 2013 alishinda tuzo ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) kama Mtunzi bora wa mashairi ya Bongo Flava.

Related Articles

Back to top button