Roma adai anaogopa kuwekeza pesa nyingi kushoot video nje
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Roma Mkatoliki amedai wasanii wengi wanaoshoot video nje kwa gharama kubwa pesa zao hazirudi kutokana na soko la muziki lilivyo.
Akizungumza na Bongo5 Jumanne hii, Roma alisema yeye binafsi hawezi kufanya biashara hiyo kwa sasa mpaka atakapo jipanga zaidi.
“Kwa kesi ya Roma ukifika muda wangu nitafanya,” alisema Roma.
“Unajua kwa sasa hivi tunaona wasanii wanaenda kushoot video kwa milioni 25 lakini kiukweli hizi pesa hazirudi. Ndio maana napenda kuwaambia wasanii wenzangu waangalie kwanza soko lao lipo wapi?, target yao ni ipi. Msanii anatoa milioni 25 kwa ajili ya kushoot video, najua itakuwa video kali lakini soko la nyumbani halitaweza kuirudisha ile pesa, kwa maana hiyo utapata hasara na hautaweza tena kushoot video nje kwa sababu hauna mtaji. Kwahiyo mimi binafsi napenda sana kwenda huko, pia nawaunga mkono wanaofanya hivyo lakini lazima tujipange na tuangalie soko letu,”