FahamuHabari

Ronaldo aanza kujenga Hoteli ya Kifahari Saudi Arabia

Mshambulizi wa klabu ya Al-Nassr na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo na mshirika/mpenzi wake Georgina Rodriguez walionyesha maendeleo ya mradi wao wa ujenzi wa hoteli yao ya kifahari katika Bahari Nyekundu/red sea huko Mashariki mwa Saudi Arabia.

Kupitia page ya Mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 30 aliandika katika Instagram yake kuwa “Building the new paradise”, akiambatanisha na video Ronaldo wakati anafanya mazoezi kipindi cha mapumziko wiki moja iliyopita.

Imeelezwa kuwa jina la Hoteli hiyo inayoitwa Visit Red Sea, iko kati ya Umluj na Alwajh na wanaahidi itakuwa sehemu ya maisha ya kufurahisha”

Mradi huo unaonekana kuwa mradi wa hivi punde wa kibiashara wa Ronaldo huko Saudi Arabia ukichukuliwa kuwa wa pamoja na mpenzi wake, huku familia yake ikiendelea kuonyeshwa kuyapenda maisha ya Saudi Arabia nchi ambayo ameiita ni kama nyumbani kwao licha ya kuwa ameishi takriban mwaka mmoja na nusu.

Tovuti nyingi ikiwemo Goal.com zimeeleza kuwa Hoteli hiyo ya Kifahari ya Ronaldo ambayo ipo kwenye kisiwa itakuwa hoteli ya kipekee kitokana na muundo wa hoteli hiyo ambayo alipost Gio.

Inaelezwa kuwa Saudi Arabia ni sehemu ambayo Ronaldo na familia yake wameipenda sana huku mtoto wake Ronaldo Junior akitajwa kuwa na furaha zaidi kuishi kwenyw taifa hilo.

Imeandaliwa na El Mando

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents