Michezo

Ronaldo ainunua timu hii inayoshiriki ligi kuu nchini Uhispani Laliga

Ronaldo ainunua timu hii inayoshiriki ligi kuu nchini Uhispani Laliga

Ronaldo Luís Nazário de Lima aliyezaliwa miaka 41 iliyopita katika jiji la Rio de Jeneiro nchini Brazil amefanikiwa  asilimia 51 ya umiliki katika timu inayoshiriki katika ligi kuu nchini Uhispania Laliga ambayo ni Real Valladolid.

Mkongwe huyo ambaye alishawahi kuichezea ligi hiyo kubwa duniani kwa zaidi ya miaka 6 akizitumikia klabu za FC Barcelona na Real Madrid huku akistaafu soka mwaka 2011,akichezea timu yake ya taifa kwa zaidi ya miaka 16 akiifungia magoli 62 na kuichezea michezo 98 ameamua kujiingiza kwenye biashara hiyo kubwa kwa sasa duniani kwa kuamua kuinunua klabu ya Real Valladolid.

Mmiliki mpya wa klabu hiyo ambaye ametambulishwa leo siku ya  Jumatatu katika mkutano wa waandishi wa habari ambapo alielezea mipango yake ya baadaye ya klabu hiyo.

Ronaldo alisema:- “Tunataka kukua na kufikia ambako mapenzi yetu yataturuhusu sisi,” aliongeza:- “Nitatumia maneno manne kuelezea siasa zetu: Ushindani, Uwazi, Mapinduzi na Jamii. Ninawahakikishia kwamba utanipata mimi nikiwa kama mpenzi na shabiki mkubwa  wa Castilla-Leon, Valladolid na Real Valladolid.”

Baada ya Ronaldo kukabidhiwa umiliki wa klabu hiyo kwa sasa akiwa na asilimia 51 ya umiliki, Ronaldo amekubali kuwa Rais aliyemkuta wa klabu hiyo Carlos Suárez atabakia katika nafasi yake, wakati mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2006 atachukua nafasi ya Rais wa Bodi ya Wakurugenzi.

 

By Ally Juma

Related Articles

One Comment

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents