
Mashabiki wa soka Iran, wameonekana kwa wingi wakiliandama Basi la wachezaji wa Al-Nassr akiwemo staa Cristiano Ronaldo ambao wapo nchini humo kwaajili ya mchezo wao dhidi ya Persepolis Michuano ya Asian Champions League.
Klip ya video imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonesha mashabiki hao wakilifukuza basi hilo katika mitaa wakati lilipotoka kwenye Hotel waliyofikia huku wakipiga kelele za Ronaldo.
Al-Nassr itawakabili Persepolis Mchezo wa Asian Champions League leo September 19.
Video Bofya HAPA